Zahera apania kuongeza pumzi ya wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Sep 2018
Zahera apania kuongeza pumzi ya wachezaji Yanga
Yanga imeendelea kujifua mkoani Morogoro huku kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera akitilia mkazo mazoezi ya kuongeza pumzi.

Asubuhi leo Jumatano, Yanga wamefanya mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri, ambapo kocha Zahera ameonekana akianza na mazoezi ya kuongeza pumzi.

Katika mazoezi hayo Zahera ameonekana akiwanya wachezaji wake katika makundi mawili moja likisimamiwa na mwenyewe huku lingine likisimamiwa na msaidizi wake, Noel Mwandila.

Kocha Zahera ameonekana kutaka kuona mchezaji anakimbia kwa kufuata muda aliotaka yakiwa ni mazoezi ya mbio za kasi.

Kila mchezaji alihudhuria mazoezi hayo isipokuwa makipa pekee ambao walikuwa na mazoezi yao na kocha wao Juma Pondamali.

Mpaka sasa Yanga inaonekana haina mchezaji majeruhi ukiondoa Juma Abdul na Juma Mahadhi ambao bado hawajajiunga na timu hiyo.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’