kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omary Kaya jana alimtembelea msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ambaye juzi alikumbwa na maradhi ya tumbo yaliyopelekea akimbizwe Hospitalini baada ya kuzidiwa.
Manara ambaye baba yake Kitwana Manara 'Computer' ni mkongwe, Yanga Damu aliyeacha historia Jangwani, amesema Kaya alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kumtembelea nyumbani kwake baada ya kutoka Hospitalini jana.
"Sijui lini ntaeleweka ninaposema Simba na Yanga si maadui wala mahasimu, fikiria miongoni mwa watu wa mwanzo kuja kwangu kuniona baada ya kutoka hospitali ni swahiba wangu ambaye ndiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaya.
"Tumeongea na kutaniana lakini pia kushauriana yenye faida kwa mpira wa Tanzania.
"Mashabiki maandazi jifunzeni kwetu na kwa wachezaji, sisi hatuna uadui, msitukanane wala kukunjana, charurareni bila kugombana" alisema Manara
Kuugua kwake maradhi ya tumbo kumepelekea ataniwe kuwa ameshikwa na maradhi hayo baada ya kusikia mshambuliaji Amissi Tambwe ametupia mabao mawili uwanja wa Taifa juzi.
Tambwe amekuwa na kawaida ya kufunga kila anapokutana na Simba kwenye uwanja huo.
Msimu uliopita hakupata nafasi ya kucheza mchezo wowote dhidi ya Simba kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu.
Lakini sasa anayo nafasi ya kuendeleza rekodi yake ya kuwafunga kwenye mchezo wa Jumapili.

ADVERTISE HERE