Hatupumzishi mchezaji bila sababu - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2018
Hatupumzishi mchezaji bila sababu - Zahera
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametaja sababu za kutowatumia baadhi ya wachezaji kwenye mchezo wa jana dhidi ya Singida United ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Zahera amesema baadhi ya wachezaji hakuwatumia kutokana na sababu mbalimbali.

"Mimi sipumzishi mchezaji bila sababu. Kamusoko aliumia juzi mazoezini wakati akiwa kwenye harakati za kupiga kona. Ngasa nae ni mgonjwa alipatwa na malaria. Alianza kuumwa baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union."

"Makambo aliumia kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Alianza mazoezi jana (juzi) lakini Daktari wa timu akatushauri ni vyema tukampumzisha ili aweze kupona kabisa."

Akizungumzia mabadiliko upande wa mlinda lango, Zahera amesema alimpa Kakolanya nafasi jana baada ya kujiridhisha yuko 'fit'

"Kakolanya sikuweza kumtumia kwenye michezo miwili iliyopita kwa kuwa hakuwa na mazoezi ya kutosha," amesema.

"Alipotoka Uganda na timu ya Taifa alichelewa kuanza mazoezi.

"Lakini pia Kindoki alifanya kosa moja kwenye mchezo dhidi ya Stand United. Kumsaidia kumjenga kisaikolojia ilikuwa ni lazima acheze mchezo dhidi ya Coastal Union."

"Huwezi kumuweka mchezaji nje kisa amefanya kosa moja kwenye mchezo uliopita. Tukianza kufanya hivyo kila siku tutakuwa tunabadilisha timu kwani wachezaji wote wanafanya makosa," amesema Zahera
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’