Tambwe hana presha mechi ya watani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2018
Tambwe hana presha mechi ya watani
Baada ya kuifungia Yanga mabao mawili jana dhidi ya Singida United, mshambuliaji Amissi Tambwe amesema hana presha yoyote kuelekea mchezo dhidi ya Simba Jumapili ijayo.

"Nashukuru mungu leo tumeweza kupata ushindi na kuondoka na alama zote tatu muhimu sasa tunajiandaa kwa ajili ya mchezo unaofuata," amesema Tambwe.

"Kwangu mimi mchezo dhidi ya Simba ni mwepesi kuliko michezo mingine. Ni kawaida kwa timu ndogo kukamia zinapokutana na Yanga lakini najua hali itakuwa tofauti mchezo dhidi ya Simba.

"Tunajua haitakuwa kazi rahisi lakini naamini tukijituma tunaweza kuibuka na ushindi."

Tambwe amerejea kwenye kikosi cha Yanga akianza kwenye mchezo wa jana baada ya kocha Mwinyi Zahera kumpumzisha Heritier Makambo.

Mabao yake mawili yanamfanya kuingia kwenye orodha ya vinara 10 wa mabao katika ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’