Mabingwa wa kihistoria wa soka Tanzania Yanga leo wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Singida United kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa kuanzia saa moja usiku.
Yanga ambayo imeshinda michezo yake yote mitatu ya mwanzo itakuwa inatafuta alama nyingine tatu kuendeleza rekodi ya ushindi kwa asilimia 100.
Viingilio vya mchezo huo; VIP A 15,000/- VIP B na C 10,000/- huku upande wa mzunguuko ikiwa 5,000/-
Kwenye mchezo huo wa leo Yanga itamkosa nahodha wake Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Pia bado Juma Mahadhi na Baruani Akilimali watandelea kukosekana kwa kuwa hawajapona majeraha yao.
Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul yeye alisharejea kikosini na hatma ya kucheza au la itabaki kwa mwalimu Mwinyi Zahera.
Ushindi kwenye mchezo wa leo utaifanya Yanga ifikishe alama 12 na inaweza kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi ambayo sasa inaongozwa na Mbao FC yenye alama 10 baada ya kushuka dimbani mara tano.
Michezo yote inayopigwa leo

ADVERTISE HERE