Matokeo ya 8-0 ya mwaka 2015 kujirudia uwanja wa Taifa leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Sep 2018
Matokeo ya 8-0 ya mwaka 2015 kujirudia uwanja wa Taifa leo?
Kipigo hicho Coastal Union walikipata kwenye mchezo wa ligi Aprili 8 2015 katika uwanja Taifa ambapo Amisi Tambwe wakati huo akiwa kwenye 'form' alifunga mabao manne peke yake.

Saimon Msuva ambaye sasa anakipiga Difaa El Jadida ya Morocco alipachika mabao mawili, Mliberia Kpah Sean Sherman na kiungo msomi aliyestaafu soka Salum Telela, nao wakifunga bao moja moja.

Yanga imekuwa na rekodi nzuri kila inapocheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Taifa huku Coastal nayo ikiwa na rekodi nzuri dhidi ya Yanga inapocheza dimba la Mkwakwani.

Mchezo wa mwisho kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union uliopigwa kwenye dimba la Taifa Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakati mchezo wa mwisho uliopigwa dimba la Mkwakwani Coastal Union iliibuka na ushindi kama huo.

Yanga imedhamiria kushinda michezo yake yote 12 inayopigwa mfululizo kwenye uwanja wa Taifa. Ushindi dhidi ya Coastal leo utafanya ifikishe alama tisa na kuwa imeshinda michezo mitatu huku ikisubiri mingine tisa
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’