Zahera ataka kujiridhisha na uwezo wa Kitenge

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
19 Sep 2018
Zahera ataka kujiridhisha na uwezo wa Kitenge
Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameoneshwa kukunwa na soka la mshambuliaji wa Stand United Alex Kitenge na haikushangaza mara baada ya pambano hilo alimsaka Uwanja wa Taifa na kufanya naye mazungumzo mafupi na ya siri akimchombeza atue Yanga.

Kitenge alifunga mabao yote ya Stand wakati timu yake ikifa kibingwa kwenye Uwanja wa Taifa, jambo lililomfanya Zahera amsake na kuzungumza naye huku akibadilishana namba zao za simu kwa mawasiliano zaidi.

Zahera amesema mshambuliaji huyo ana uwezo mkubwa wa kupachika mabao.

“Mastraika wa aina hii ya Kitenge ndio natamani kuwa nao katika timu yangu, nilikuwa namfahamisha ana uwezo wa kucheza Yanga kama atakuwa na kasi hiyo ya kufunga mpaka wakati wa dirisha dogo nitawapatia jina hilo Kamati ya Usajili.

“Nitaendelea kumfuatilia mechi za Stand msimu huu ili kuona uwezo wake zaidi wa kufunga kama alivyofanya katika mechi yetu na msaada wake ndani ya timu na nimefungua mawasiliano naye, ikibidi aje kucheza Yanga.”

Kocha Zahera alisema kwa kuwa timu yake itasajili straika dirisha dogo ili kuongeza nguvu na aina ya washambuliaji anaowataka ni kama kina Kitenge wenye jicho la kufunga.

“Angalia hata bao lake la kwanza alivyofunga akiwa na beki na alilazimisha kupiga shuti, lakini hata mabao mengine mawili yote ni umakini wa hali ya juu alionao katika kufunga,” alisema.

Kitenge aliyewahi kufunga hat-trick alipokuwa akiichezea AFC Leopard walipocheza na Gor Mahia, alisema kufunga mabao sio kitu kigeni na kukiri kuhitajiwa na Zahera Jangwani.

“Maneno aliyoniambia kocha wa Yanga Zahera ni kwamba atanifuatilia zaidi na kama nitafanya vizuri zaidi kwa kufunga magoli na kutoa msaada ndani ya timu anawezaa kunisajili wakati wa dirisha dogo.

“Maneno hayo yataniongeza morali ya kujituma zaidi ingawa nilikuja hapa nchini nikiwa na malengo hayo na kutamani kuwa mfungaji bora pia,” alisema Kitenge.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →