Azam TV kutoa tiketi 250 za VIP bure mpambano wa watani wa jadi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
18 Sep 2018
Azam TV kutoa tiketi 250 za VIP bure mpambano wa watani wa jadi
Mkurugenzi wa Masoko wa Azam Media Abdul Mohamed amesema kuwa Azam TV imeandaa ofa ya tiketi 250 za VIP kwa watumiaji wa ving’amuzi vya Azam TV kwaajili ya kwenda uwanjani kutazama mechi kubwa ya Simba na Yanga itakayopigwa Jumamosi ya tarehe 30/09/2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye Mkutano ambao pia ulihudhuriwa na wasemaji wa vilabu vya Simba na Yanga, Abdul amewataka wale ambao ving'amuzi vyao vina matatizo wachangamkie ofa maalum kwa ajili yao.

"Kama una king’amuzi kibovu kilete, na Azam TV itakupa king’amuzi kingine, kwa sharti moja la kulipia kifurushi chako cha Pure kwa miezi minne," amesema Abdul

"Pia kama rimoti yako inasumbua, ilete tutakupa mpya kwa sharti la kulipia kifurushi chako cha pure kwa miezi miwili."

Naye Meneja wa Michezo wa Azam Media, Baruan Muhuza amesema wamejipanga kuhakikisha mchezo huo utakuwa katika muonekano bora kuwapa wateja wao burudani ya uhakika.

"Matangazo ya mchezo kati ya Simba na Yanga yatakuwa na ubora wa hali ya juu na tumejipanaga kuondoa kila aina ya utata unaoweza kuwepo kama ambavyo imeonekana kwenye mechi za msimu huu," amesema.



Wasemaji wa vilabu vya Simba na Yanga, Haji Manara na Dismas Ten wamesema timu zao zimejipanga kikamilifu kuhakikisha zinaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

"Mashabiki wa Simba njooni kwa wingi uwanja wa Taifa Septemba 30 tujaze robo tatu ya uwanja ili kuipa nguvu timu yatu siku hiyo iweze kuibuka na ushindi mnono," amesema Manara.

Naye Dismas Ten Afisa habari wa Yanga amesema timu yake imejipanga kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo.

“Maandalizi ya mechi kama hii ni tofauti na maandalizi ya mechi nyingine. Sisi tumejiandaa kiutofauti na tuko tayari kwa ajili ya mchezo huo," amesema
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →