TFF yaja na mkakati wa kufuzu AFCON 2019

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
17 Sep 2018
TFF yaja na mkakati wa kufuzu AFCON 2019
TAARIFA YA TFF KWA VYOMBO VYA HABARI

Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” itacheza mchezo wake wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Cape Verde Oktoba 12,2018 na mchezo wa marudiano utachezwa Uwanja wa Taifa Oktoba 16,2018.

TFF kwa kushirikiana na Wadhamini wa Taifa Stars Bia ya Serengeti Premium Lager tunafanya utaratibu wa usafiri utakaoipeleka na kuirudisha timu ya Taifa kulingana na ratiba ya michezo hiyo ilivyokaa.

Utaratibu wa Kambi/Kikosi Walimu watauzungumza ambao utazingatia umuhimu wa mchezo,tarehe za kuondoka na tarehe za michezo yote miwili.

Unafanyika utaratibu wa kusafiri na mashabiki wa timu ya Taifa ambao watachangia gharama kidogo.

Tumekuja na Hashtag itakayotumika katika safari yetu ya kutupeleka Cameroon kwenye fainali hizo za mwakani #AfconCameroon2019ZamuYetu

Rai yetu kwa Vyombo vya Habari tuungane pamoja kwakuwa ni sehemu muhimu katika safari hiyo ya kwenda Cameroon,Wadau mbalimbali tuungane pamoja Tanzania ni yetu,Taifa Stars ni timu yetu.

Msimamo ulivyo mpaka sasa tunayo nafasi ya kwenda Cameroon kwenye Fainali za Afcon.

Uganda wanaongoza wakiwa na alama 4 ,Lesotho na Tanzania wana alama 2 na Cape Verde wakiwa na alama 1.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7m ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →