Makambo awatia kiwewe Stand United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2018
Makambo awatia kiwewe Stand United
Mshambuliaji hatari wa Yanga Heritier Makambo amemtia kiwewe kocha wa Stand United Athumani Bilali 'Bilo' kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara baina ya timu hizo utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.

Makambo tayari amepachika bao moja kwenye ligi msimu huu katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar huku bao lake jingine likikataliwa na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo kufungiwa.

Bilo amesema Makambo ni miongoni mwa washambuliaji bora kwenye ligi na watahitaji kujipanga ili waweze kumdhibiti

"Nimewapa kazi maalumu walinzi wangu kuhakikisha wanatembea nae popote aendapo ili asilete madhara," amesema Bilo

Makambo ndio mshambuliaji anayeogopwa zaidi na walinzi wa timu pinzani kwenye ligi ambapo baada ya kuonyesha kiwango cha hali ya juu amekuwa akikamiwa sana.

Kwenye moja ya mahojiano yake Makambo alisema walinzi wa timu pinzani wamekuwa wakimkamia na kumfanyia rafu kwa lengo la kutaka kumuumiza.

Lakini amesema yeye ni mshambuliaji na alitarajia matukio kama hayo kutoka kwa wapinzani wake.

"Mimi kazi yangu ni kupachika mabao. Changamoto ya kukamiwa na walinzi wa timu pinzani nimeizoea na nitandelea kufunga kila nitakapopata nafasi," amesema.

Uwezo wake wa kutumia miguu yote, uhodari katika kumiliki mpira na kufunga kwa kichwa umemfanya kuwa mshambuliaji wa kuogofya kwenye ligi msimu huu
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’