Kikosi cha Yanga leo asubuhi kimeendelea kujifua uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Stand United utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.
Mabingwa hao wa kihistoria Tanzania wataingia katika mchezo huo kuwania alama tatu muhimu katika kampeni ya kutwaa ubingwa msimu huu.
Ari ya wachezaji wa Yanga iko juu na wamepania kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo unaofungua mfululizo wa michezo 11 itakayopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Kulingana na Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, timu hiyo haina majeruhi wapya zaidi ya Juma Mahadhi anayeuguza majeraha ya goti.
Msimu huu michezo yote ya Yanga ina umuhimu wa kipekee, Hafidh amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu yao ili iweze kuibuka na ushindi.
Yanga haipaswi kupoteza alama hata moja kwenye michezo yake yote inayopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

ADVERTISE HERE