Takwimu zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Stand United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Sep 2018
Takwimu zaibeba Yanga mchezo dhidi ya Stand United
Keshokutwa Jumapili Septemba 16 mabingwa wa Kihistoria wa Tanzania Bara Yanga watashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya nne.

Yanga itakuwa inashuka dimbani mara ya pili msimu huu baada ya michezo yake miwili kuahirishwa kutokana na sababu ya muingiliano wa ratiba.

Katika misimu mitatu iliyopita Yanga na Stand United zimekutana mara sita kwenye ligi Yanga ikifanikiwa kuibuka na ushindi mara tano huku Stand ikishinda mara moja mwaka 2016.

Msimu ulioipita Yanga iliifumua Stand United mabao 4-0 kwenye mchezo wa raundi ya kwa kwanza uliopigwa mkoani Shinyanga kabla ya kushinda mabao 3-1 timu hizo ziliporudiana jijini Dar es salaam.

Msimu huu Stand United tayari imeshuka dimbani mara tatu, imeshinda michezo miwili na kufungwa mchezo mmoja ikiwa na alama sita.

Yanga imekuwa ikipata matokeo mazuri kila inapocheza dhidi ya Stand United na wengi wana matumaini kuwa Wana Jangwani hao wataendeleza utaratibu huo wa kuwapa raha mashabiki wao kwenye uwanja wa Taifa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’