Pichani Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga,
Hussein Nyika
Jana moja ya habari kubwa kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa kuhusu mlinzi wa kati wa Simba Juuko Murshidi akidaiwa kurejea timu hiyo huku ikisemekana eti alitaka kusajiliwa na Yanga.
Ukweli ni kwamba Yanga haikuwahi kuwa na mpango wa kumsajili mchezaji huyo kulingana na taarifa tuliyopewa na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya usajili ya Yanga.
Kilichotokea ni magazeti kama ilivyo kawaida yao ya kutengeneza habari ili waweze kuyauza mtaani lakini jambo hilo halikuwepo.
Wachezaji wa Kimataifa waliokuwa wasajiliwe na Yanga wanafahamika, Juuko hakuwahi kuwa mmoja wao.
Mchezaji huyo alikuwa Afrika Kusini kufanya majaribio kwenye klabu ya Orlando Pirates lakini alishindwa hivyo kumlazimu arejee Simba kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Usajili wa msimu huu umetufunza jambo, tusiamini kwa asilimia 100 yale tunayoyaona kwenye magazeti ya michezo wengine wanatengeneza habari ili kuuza magazeti yao.
Sasa Yanga ina Afisa wa Habari makini, Dismas Ten ambaye hutoa kwa wakati kila taarifa muhimu ya klabu. Tuendelee kuwaamini viongozi wetu kwani wao ndio chanzo sahihi cha habari.

ADVERTISE HERE