Zahera amtaka Straika kutoka Burkina Faso

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2018
Zahera amtaka Straika kutoka Burkina Faso
Kama kuna kitu ambacho mashabiki wa Yanga wanacheka kwa sasa ni kazi nzuri iliyofanywa na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Mwinyi Zahera katika kuwaletea wachezaji wa maana tangu atue Jangwani.

Katika muendelezo ule ule wa kuifanya Yanga iwe moto zaidi, Mkongo huyo amewasilisha ombi kwa mabosi wake akitaka aletewe straika matata, Ahmed Toure raia wa Burkina Faso anayekipiga Asec Mimosas ya Ivory Coast.

Kocha Zahera katika maombo yake aliwataka mabosi wake, kumletea straika mmoja au wawili wa maana, ili waungane na Heritier Makambo ndipo jina la Toure likaibuka na haraka Yanga wameanza mipango ya kumleta dirisha dogo.

Straika huyo mwenye miaka 31 akiwa na urefu wa futi 6 na inchi 2 na aliyewahi kukipiga Asante Kotoko ya Ghana alionwa na Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na jamaa anajua kucheka na nyavu.

Ingawa Yanga inafanya siri, lakini Mwanaspoti linafahamu kwamba Bosi wa Usajili Hussein Nyika amemtuma kigogo mmoja katika kamati yake kwenda kufanya mazungumzo na straika huyo aliyerudi klabu kwake akitoka kuitumikia taifa lake katika mechi za kimataifa wikiendi iliyopita.

Hata hivyo, upinzani mkubwa kwa Yanga ni kumshawishi mshambuliaji huyo kuikubali Yanga kuachana na ofa ya nchini Iceland aliyoipata ambapo moja ya klabu ya huko imemtaka kusubiri mpaka Novemba kumtumia tiketi aende huko.

Inaelezwa kwamba mbali na Toure kamati ya Nyika ina majina matano ambayo ndani yake kuna washambuliaji hatari kama alivyo Toure.

Kufuatia taarifa hizo Mwanaspoti lilimtafuta Nyika kujua ukweli wa hilo ambapo alishindwa kukubali au kukataa akisema bado wanaendelea kukifanyia maboresho kikosi chao lakini kwasasa hawawezi kusema lolote juu ya Toure.

β€œTunaendelea kufanya maboresho katika kikosi chetu lakini sio kila kitu kinatakiwa kutolewa kwanza hadharani, huyo Toure siwezi kuweka wazi chochote kwasasa,” alisema Nyika na kukata simu.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’