Kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United utakaopigwa Jumapili, Septemba 16 kwenye uwanja wa Taifa, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo.
Afisa Habari Msaidizi wa Yanga Godlisten Anderson 'Chicharito' amesema Yanga inatarajiwa kuingia kambini leo baada ya mazoezi ya jioni.
Majeruhi amebaki mmoja
Wakati huo huo Chicharito amesema wachezaji wote wa Yanga waliokuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa na wengine waliokuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi.
Mchezaji pekee ambaye bado ni majeruhi ni kiungo Juma Mahadhi.
Wachezaji ambao walikuwa majeruhi na wameanza mazoezi jana ni pamoja na nahodha Kelvin Yondani, Juma Abdul na Abdallah Shaibu.

ADVERTISE HERE