Yanga huwa inafanikiwa hapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Sep 2018
Yanga huwa inafanikiwa hapa
Yanga ya msimu huu imejaaliwa kuwa na wachezaji vijana wenye vipaji vya hali ya juu.

Licha ya changamoto za kiuchumi zilizoikumba Yanga msimu uliopita, mabosi wa timu hiyo chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu Charles Mkwasa walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye usajili.

Mwaka jana Yanga ilisajili vijana wengi kama Abdallah Shaibu, Pius Buswita, Raphael Daudi, Yohana Mkomola, Ramadhani Kabwili, Gadiel Michael, Ibrahim Ajib na Baruani Yahya huku pia ikiwapandisha kikosi cha kwanza Maka Edward na Said Mussa.

Hao wakaja kuungana na wachezaji wengine vijana waliokuwa kikosini kama Benno Kakolanya, Juma Abdul, Said Juma, Pato Ngonyani, Andrew Vicent 'Dante', Emanuel Martin, Juma Mahadhi, Yusufu Mhilu na Geofrey Mwashiuya ambaye kwa sasa ametimkia Singida United

Msimu huu Yanga imewaongeza Feisal Salum, Klaus Kindoki, Mohammed Issa 'Banka', Jaffar Mohammed na Heritier Makambo huku ikiwarejesha wazoefu Deus Kaseke na Mrisho Ngassa.

Wachezaji hawa vijana wanaweza kuwa hawakuisaidia sana Yanga msimu uliopita lakini hakuna shaka matunda ya uamuzi wa kuwasajili yataonekana msimu huu na misimu ijayo.

Moja ya sifa kubwa ya Yanga ni kuwa na mipango endelevu. Ukifuatilia kuanzia mwaka 1990, Yanga imebeba taji la ligi kuu mara tatu mfululizo katika vipindi vitatu tofauti.

Mwaka 1991, 92, 93 halafu 1996, 97, 98 ikarudia tena 2015, 16 na 17. Hakuna timu nyingine iliyofanya hivyo kwenye kipindi hicho.

Yanga imewahi kutwaa taji la ligi kuu kwa misimu mitano mfululizo kuanzia mwaka 1967 hadi mwaka 1972 ingawa Simba nayo ikafanikiwa kuijibu rekodi hiyo kuanzia mwaka 1975 mpaka mwaka 1980.

Lakini rekodi muhimu zaidi ni kwamba katika kipindi cha miaka 13 iliyopita, Yanga haijawahi kukaa zaidi ya msimu mmoja bila ya kutwaa ubingwa.

Ni mipango tu hasa wakati wa usajili ndiyo inayoifanya Yanga iwe na rekodi za kutisha linapokuja swala la ubingwa.

Kwa kikosi hiki ambacho Yanga inacho sasa, inaweza kuchukua ubingwa hata kwa misimu mitano mfululizo kama kitatunzwa vyema.

Kwani ndani ya kikosi cha Yanga cha sasa wachezaji ambao unaweza kusema huenda wasiwepo kikosini baada ya misimu mitatu au minne kutokana na umri wao hawazidi watano.

Huwezi kufananisha na kikosi kama cha Simba ambacho idadi kubwa ya wachezaji wao ni wakongwe. Kwa timu kama Simba kuchukua ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo ni ndoto!

Idadi kubwa ya wachezaji wa Yanga umri wao upo kati ya miaka 18 na 26.

Baada ya kuifundisha Yanga kwa miezi mitatu, kocha Mkuu Mwinyi Zahera alikiri kuwa ameshuhudia vipaji vya hali ya juu.

Alisema msimu uliopita ulikuwa mgumu kwa sababu wengi wa wachezaji hao walikosa uzoefu na kujiamini lakini sasa wengi wameanza kuimarika na kuongeza kujiamini.

Zahera amesema kikosi hiki cha Yanga kinaweza kutwaa ubingwa msimu huu jambo la msingi ni viongozi wa timu hiyo kufanyia kazi mapendekezo yake ya kuongeza wachezaji sehemu zenye upungufu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’