FT : Yanga 1-0 African Lyon

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Sep 2018
FT : Yanga 1-0 African Lyon
Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya African Lyon uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa umemalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo maalum kwa ajili ya kupiga vita ujangili wa meno ya tembo, uliishuhudia Yanga ikipata bao lake kwenye dakika ya 83 mfungaji akiwa Yusufu Mhilu aliyeunganisha kwa kichwa mpira uliotemwa na mlinda lango wa African Lyon kufuatia krosi ya Matheo Anthony.

Ikiwatumia vijana watatu chipukizi kwenye safu ya ulinzi kutoka kikosi cha pili, Paul Godfey, Gustapha Simon na Cleofas Sospeter, vijana hao waliweza kumudu mikiki mikiki ya mchezo huku Yanga ikifanikiwa kutawala kwa muda mwingi.

Mrisho Ngasa aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Yanga leo nusura afunge bao kwenye kipindi cha kwanza kama si mpira wake wa kichwa kugonga mwamba.

Hadi wakati wa mapumziko hakukuwa na timu iliyokuwa imefunga ambapo mapema kwenye kipindi cha pili Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Pius Buswita ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Matheo Anthon wakati Papi Tshishimbi aliingia kuchukua nafasi ya Raphael Daudi.

Wengine walioingia baadae kwenye kipindi cha pili ni pamoja na Amissi Tambwe, Yusufu Mhilu, Jaffar Mohammed na Ibrahim Ajib kuchukua nafasi za Heritier Makambo, Gustapha Simon, Deus Kaseke na Mrisho Ngasa.

Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga ambacho wiki ijayo Septemba 16 kitashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Stand United katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’