Kikosi cha mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga leo kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili African Lyon katika mchezo wa kirafiki maalumu kwa ajili ya kupiga vita ujangili wa meno ya tembo.
Mchezo huo ambao pia utatumika kuziandaa timu zote kabla ya kurejea mikiki mikiki ya ligi kuu ya Tanzania Bara wiki ijayo, unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni.
Viingilio vya mchezo huo;
VIP A 100,00/-
VIP B&C 5,000/-
Mzunguko 3,000/-
Watoto 1,000/-
Yanga itaingia katika mchezo huo bila ya wachezaji wake saba wanaokosekana kutokana na sababu mbalimbali.
Wakati Beno Kakolanya, Gadiel Michael na Andrew Vicent wakiwa na kikosi cha timu ya Taifa, Kelvin Yondani, Juma Abdul, Juma Mahadhi na Abdallah Shaibu watakosekana kutokana na majeruhi.
Aidha kiraka Pato Ngonyani nae huenda akaukosa mchezo huo baada ya hapo jana kukamilisha tukio maalumu la kihistoria baada ya kufunga ndoa.

ADVERTISE HERE