Wala si jambo la kushitusha kwa WanaYanga wanaposikia shughuli inayofanywa na Simon Msuva huko ughaibuni akiichezea klabu ya Difaa El Jadida, ya Morocco.
Kwa misimu mitano aliyokuwa Yanga Msuva ameibuka mfungaji bora wa VPL mara mbili na ameondoka Yanga akiwa amefunga zaidi ya mabao 60.
Tayari ameichezea klabu yake hiyo mpya michezo nane ya kirafiki na ameshafunga mabao sita.
Jana ameifungia Difaa bao moja katika mechi yake ya nane ambayo DHJ ilifungwa 2-1 na timu ya Daraja la Kwanza, Union Sportive Musulmane Oujda (USMO) Uwanja wa El Abdi mjini Jadida.
Tunaendelea kumtakia kila la kheri, mafanikio yake yatatengeneza uhusiano mwema kati ya Yanga na DHJ ambayo huenda ikatamani kurudi tena Jangwani.
Usajili wa Msuva umeiingizia Yanga zaidi ya Mil 300 ambazo naamini zimetumika vyema kukiimarisha kikosi cha Yanga.
Japo ni lazima tukiri kuwa kumpoteza mchezaji wa kiwango chake ni pigo lakini soka sasa ni biashara, wachezaji wazuri wamekuwa bidhaa ghali.
Naamini vijana waliopo kikosini wataweza kumudu nafasi aliyokuwa anacheza Msuva.

ADVERTISE HERE