Niyonzima amvulia kofia beki kisiki anayenyemelewa na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
9 Sep 2018
Niyonzima amvulia kofia beki kisiki anayenyemelewa na Yanga
Usajili wa Yanga msimu huu umekuwa wa kiufundi zaidi kiasi cha kuwapa mzuka mashabiki wake kwamba, wanaweza kupambana na Simba ambao, wamejipambanua kuwa matajiri na wababe kwenye Ligi Kuu Bara.

Yanga sasa imeanza kurejea kwenye anga zake taratibu huku usajili wake iliyofanya, ukionekana kuwatisha watani zao, ambao kwa sasa wanaogelea kwenye utajiri wa bilionea wao, Mohamed Dewji (MO) ambaye amewekeza fungu la maana.

Lakini, ishu kubwa kwa sasa ndani ya Yanga ni mchakato wa kumvuta beki kisiki wa Rayon Sport na timu ya Taifa ya Rwanda, Abdoul Rwatubyaye, ambaye tayari imeelezwa kuwa atakuja kutengeneza ukuta wa Berlin akicheza sambamba na nahodha, Kelvin Yondani.



Mabosi wa Yanga akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ambao waliongozana na kikosi cha kocha Mwinyi Zahera kwenye mchezo wa mwisho kule Kigali, Rwanda, tayari wameanza kuweka mambo sawa huku wakisubiri ruhusa tu ya benchi la ufundi kabla ya kumaliza mchezo.

Hata hivyo, wakati mambo yakiwa hivyo, kiungo fundi wa mpira ambaye hatima yake bado kitendawili kwenye kikosi cha Mbelgiji, Patrick Aussems, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, amesema kwa beki huyo Yanga watafurahi wenyewe.

Niyonzima ambaye anacheza na beki huyo kwenye timu ya Taifa ya Rwanda, Amavubi, amesema kama kweli mabosi wa klabu yake hiyo ya zamani watanasa huduma ya Rwatubyaye, basi watakuwa wamelamba dume kwani, jamaa anakaba hadi aibu.

Rwatubyaye anatajwa kuwa ni mahiri wa kucheza soka la kibabe na kudhibiti washambuliaji wakorofi, ndiye alimficha vilivyo straika matata wa Yanga, Heritier Makambo kwenye mchezo huo na mabosi wa Jangwani wakaona itakuwa vyema kama akisimama na Yondani kumlinda Clatus Kindoki au Beno Kakolanya.

Mabosi wa Yanga wanaamini kwamba, Mnyarwanda huyo anaweza kuongeza kitu cha ziada katika ulinzi akiwa na Yondani katika kuwadhibiti Meddie Kagere na Emmanuel Okwi, ambao kwa sasa ni balaa tupu kwenye Ligi Kuu Bara.

Pia, Rwatubyaye ambaye ni nahodha wa Rayon Sports, ana uwezo mkubwa sio kwa kuzuia tu, bali kuanzisha mashambulizi, kucheza mipira ya juu na chini na kuleta utulivu mchezoni.

“Huyu Rwatubyaye ni mzuri sana na tuko naye kwenye kikosi cha Amavubi, sio mtu wa mchezo mchezo kabisa. Anaweza kwenda vizuri na kasi ya soka la Bongo kwa kiwango chake uwanjani.

Kama Yanga wako siriasi basi ni mtu sahihi na atawasaidia sana kuimarisha kikosi chao,” alisema Niyonzima, ambaye amesisitiza kwa sasa akili yake ipo kwa Amavubi.

Kwa sasa ukuta wa Yanga unalindwa na Yondani akicheza na pacha wake Andrew Vincent ‘Dante’ baada ya Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu na kupewa ubosi klabuni hapo.

Kwa upande wake, Rwatubyaye amekiri kufanya mazungumzo na mabosi wa Yanga kwa dakika kadhaa baada ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika na kubadilisha mawasiliano.

Pia, amesema kuwa anafahamu bado ana mkataba na Rayon Sport, lakini hilo haliwezi kumzuia kama Yanga watafikia makubaliano na klabu yake nay eye mwenyewe.

“Ni kweli tumefanya mazungumzo mafupi na wameonyesha nia ya kutaka huduma yangu, lakini kila kitu kina mwanzo wake,” alisema mwenye miaka 21 kwa sasa licha ya kuwa na umbo kubwa.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera naye alikaririwa akisema: “Nahitaji beki imara, ambaye anaweza akasimama na Yondani mwenye kuhimili mikiki mikiki.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →