Kila la kheri Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Sep 2018
Kila la kheri Stars
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo kinashuka kwenye uwanja wa Mandela huko Kampala kuwakabili wenyeji wao Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019.

Stars iliwasili nchini Uganda juzi na jana jioni ikafanya mazoezi kwenye uwanja wa Mandela utakaotumika kwenye mchezo mchezo huo.

Licha ya takwimu kuibeba zaidi Uganda, Stars ina nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo kutokana na ubora wa kikosi chake.

Stars itaongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta ambaye yuko katika kiwango kizuri cha upachikaji mabao akiwa anafanya vizuri na timu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Lakini pia wapo akina Thomas Ulimwengu, Simon Msuva, Shabani Iddi Chilunda na Himid Mao miongoni mwa wachezaji tisa wanaosaka soka la kulipwa katika kikosi cha Stars.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike amesema wamekwenda nchini Uganda kushinda na wamejipanga kikamilifu kulifanikisha hilo

Ushindi au hata matokeo ya sare yatakuwa na faida kwa Stars ambayo inacheza mchezo huo ugenini.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa kumi kamili jioni na utaonyeshwa mubashara na ZBC2 pamoja na DSTV.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’