Wakati wenzie wakibweteka, Julio amewatahadharisha

Yanga Damu By Yanga Damu
•
14 Aug 2017
Wakati wenzie wakibweteka, Julio amewatahadharisha
Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo 'Julio' ametofautiana na mashabiki wa klabu ya Simba wanaoibeza safu ya ulinzi ya Yanga kwa kuwaambia wanajidanganya kwa kudhani Yanga ni nyepesi hivyo.

Julio kocha mwenye uzoefu wa soka la bongo ambaye pia ni mnazi mkubwa wa Simba amenukuliwa na gazeti la Mwanaspoti akisema Yanga inaweza ikafanya kisichotarajiwa na wengi August 23.

“Simba, wasije wakajibweteka wakidhani, beki ya Yanga ni mbovu, ninachokiona ni kocha George Lwandamina, anakiandaa kikosi chake, kujifunga dhidi ya Ruvu, siyo sababu hayo ni maandalizi tu, wapo kina Cannavaro na Yondani, wana uwezo wa juu na wazoefu.

“Huwezi kukibeza kikosi cha Yanga, wakati kipo kwenye maandalizi kwa sababu kocha anakuwa anampima kila mchezaji ili kujua ubora na madhaifu yake, kujifunga ni mambo ya kawaida na hilo atalifanyia marekebisho ndani ya siku 10 zilizosalia,”alisema kocha huyo wa Dodoma FC.

Julio alisema Simba , ndiyo ipo kwenye hatari zaidi tofauti na majina makubwa wanayoyaamini mashabiki kwa maana ya kikosi ni kipya kinatakiwa kukaa kwa pamoja kwa muda mrefu, ili kutengeneza kombinesheni ya wachezaji.

“Simba ni timu mpya, kocha atakuwa na kazi ngumu kuliko Yanga, ambao wengi ni wazamani wameongezeka wachache, wageni, wajipange vilivyo kuendana na uhalisia wa uwanjani na si kishabiki,”alisema Julio ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

Sifa moja ya Julio mbali na 'kelele' zake nyingi huwa sio mnafiki. Anachozungumza ni kweli kabisa.

Kwa wale wanaodhani Yanga ni nyepesi kihivyo wasubiri kujitundika August 23.

Katika michezo yote ya kirafiki Lwandamina alihakikisha kila mchezaji anapata nafasi ya kucheza ili aonekane.

Sawa mashabiki jambo wanalotaka ni ushindi lakini wakati huu Mwalimu anahitaji zaidi kujua ni mchezaji gani anaweza kufaa nafasi gani.

Na ndio maana katika michezo yote wachezaji wamekuwa wakijaribiwa kwenye namba tofauti.

Linapokuja swala la mashindano lazima Mwalimu awe tayari na kikosi cha kwanza hivyo wasitegemee Yanga iliyocheza na Ruvu Shooting au Mlandege ikawa ni hiyo hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →