Majina matatu ya wachezaji wa Yanga yametua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), huku mikataba yao nayo ikiwasilishwa katika taasisi hiyo.
Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zilizothibitishwa na kiongozi mmoja, ambaye hakupenda kutajwa jina lake, zinasema Takukuru mara baada ya kutua Yanga wameomba mikataba ya wachezaji watatu wa timu kwa uchunguzi zaidi.
Mikataba ambayo imeombwa na Takukuru ni wa winga kinda, Burhan Akilimali βKiberengeβ aliyesajiliwa msimu uliopita. Mbali na Akilimali pia Yanga imepeleka taarifa ya usajili wa beki Mkongomani, Fistoo Kayembe, ambaye alikaribia kabisa kutua Yanga.
Kayembe alisajiliwa na Yanga, lakini klabu yake ya Sangabalenge ikagoma kumwachia ikidai bado ana mkataba, hivyo kuzuia hati yake ya uhamisho (ITC).
Pia, klabu hiyo ilitaka ilipwe Dola 5000 (Sh11 milioni) kama ada ya uhamisho, lakini Yanga iligoma na kukubaliana kumsubiri amalize mkataba.
Mbali na hao pia mkataba wa kiungo kiraka, Jafary Mohamed aliyesajiliwa msimu huu akitokea Majimaji ya Songea nao umepelekwa Takukuru. Hata hivyo, inaelezwa kuwa baadhi ya vigogo wa Yanga nao wanaweza wakaitwa kujieleza juu ya mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya klabu hiyo.
Kutokana na taarifa hiyo, Mwanapoti lilimtafuta Msemaji wa Takukuru, Mussa Misalaba ambaye hakukubali wala kukataa juu ya suala hilo, lakini akasema hayuko kwenye wakati sahihi kulizungumzia.
βKwa sasa siwezi kusema hilo lipo au halipo, hatuoni kama kuna sababu ya kulitolea ufafanuzi kwa wakati huu, kama tutakuwa na kitu cha kuwaeleza tutafanya hivyo wakati ukifika,β alisema Misalaba
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE