Uongozi wa Yanga hauna kinyongo na aliyekuwa mshambuliaji wake Obrey Chirwa ambaye ameonyesha nia ya kutaka kurejea Jangwani baada ya kuamua kuvunja mkataba wake na klabu ya Nogoom El Mostakbal inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri.
Chirwa anataka kuachana na Nogoom El Mostakbal baada ya klabu hiyo kushindwa kumlipa fedha za usajili kwa mujibu wa makubaliano yao.
Taarifa ya Chirwa kutaka kurejea Yanga iliibuka mapema wiki hii baada ya mshambuliaji huyo kuwatumia viongozi wa Yanga ujumbe wa sauti akiomba kurejea hata kwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
Habari za Uhakika ni kwamba Kamati ya Usajili ya Yanga iko tayari kumpokea mshambuliaji huyo msumbufu kama Kocha Mwinyi Zahera ataridhia asajiliwe.
Wengi wanaamini safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo sasa inamtegemea Heritier Makambo itakuwa hatari zaidi kama Chirwa ataongezwa.
"Makocha wamesema ukiacha tabia yake, lakini kama dili hilo litafanikiwa Chirwa anaweza kuongeza uhai kwa Makambo kwa kumwongezea makali zaidi ya kufunga," amenukuliwa mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Usajili
βKazi ya kuifanyia tathimini pacha hiyo imeanza, unajua Chirwa ni mbishi kwa mabeki na anajua kupambana hivyo, wakati akiwania mipira kazi ya Makambo itakuwa ni kufunga tu. Ngoja tutaona hatima yake kwa Zahera,β alisema bosi huyo

ADVERTISE HERE