Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi kwenda nchini Uganda kuwakabili wenyeji Uganda Cranes kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019 itakayofanyika nchini Cameroon.
Stars imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa Taifa kujiandaa na mchezo huo ambao haipaswi kupoteza ili kuweka hai matumaini ya kufuzu baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Lesotho kwenye mchezo wake wa kwanza.
Uganda iliichapa Cape Verde bao 1-0 kwenye mchezo wake wa kwanza.
Kikosi cha Stars kimekamilika baada ya kuwasili kwa wachezaji wote wanaosakata kabumbu nje ya nchi.
Nyota wanaocheza soka la kulipwa waliojiunga katika kambi ya Stars ni nahodha Mbwana Samatta anatokea Genk ya Ubelgiji, Thomas Ulimwengu (AL Hilal, Sudan), Banda (Baroka, Afrika Kusini), Hassan Kessy (Nkana Fc, Zambia), Himid Mao ( Pertojet, Misri), Farid Mussa na Shaban Chilunda (CD Tenerifa, Hispania), na Rashid Mandawa (BDF XI, Botswana).

ADVERTISE HERE