Majeraha ya goti yamemrudisha nyuma chipukizi Yusufu Mhilu ambaye tayari alijihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga mwishoni mwa msimu uliopita.
Wakati huo Yanga ikionekana kupoteana, Mhilu alikuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa kabla ya kupata majeraha ya goti.
Baada ya kupona majeraha hayo, Mhilu amepania kurejea katika kikosi cha kocha Mwinyi Zahera lakini sasa anakabiliwa na ushindani zaidi kutokana na usajili uliofanywa na Yanga.
Uwepo wa Matheo Anthony, Deus Kaseke, Mrisho Ngasa na hata Juma Mahadhi ambaye kiwango chake kimeendelea kuimarika utamlazimu Mhilu afanye kazi ya ziada kumshawishi kocha Zahera
Mhilu alipata nafasi kwenye mchezo wa mwisho wa kombe la SHirikisho dhidi ya Rayon Sports wiki iliyopita mchezo ambao Yanga ilifungwa kwa bao 1-0 na yeye akipata majeraha mapya.
Hata hivyo Mhilu amesema majeraha aliyopata yalikuwa ya kawaida na leo anatarajiwa kurejea kikosini kuendelea na mazeozi.

ADVERTISE HERE