Tamaa imemponza Chirwa

Suleiman Sudi By Suleiman Sudi
β€’
3 Sep 2018
Tamaa imemponza Chirwa
Kilichomtokea Obrey Chirwa huko Misri ni funzo kwake pengine na kwa wachezaji wengine ambao wamekuwa wakiweka maslahi mbele bila ya kujali uhalisia wa nyakati.

Chirwa aliyetimkia Yanga na kutua timu ya Nogoom El Mostakbal FC inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri ameomba kurudi baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa fedha zake za usajili.

Chirwa aliondoka Yanga huku akiwa bado kwenye mipango ya timu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Hussein Nyika amebainisha kuwa walikuwa wamefikia makubaliano na mshambuliaji huyo kusaini mkataba mpya.

Lakini alishindwa kuwa mvumilivu kama walivyofanya wachezaji wengine.

Wakati Yanga ikisaka fedha kwa ajili ya kukamilisha usajili wake, yeye akatimkia nchini Misri kimyakimya.

Hata hivyo ni dhahiri huko alikokwenda mambo yamekuwa magumu zaidi na sasa anawaangukia viongozi wa Yanga asajiliwe hata kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Wakati mwingine ni vyema kwa mchezaji kuwa na uvumilivu.

Ni uvumilivu ndio uliowafanya akina Nadir Haroub waweze kudumua katika timu moja kwa zaidi ya miaka 12 tena wakicheza katika viwango bora kwa muda mrefu.

Kama Chirwa angevumilia kidogo tu hakuna shaka angelipwa fedha zake hata kama ingekuwa kwa awamu. Jambo la msingi kwake ilikuwa kufahamu mazingira ya timu kwa wakati huo.

Sasa amesikia akina Manji wamerudi huku WanaYanga wakiijaza timu yao 'mapesa' kwa kuichangia kila mwezi anaomba kurudi.

Kama mimi ningekuwa kiongozi wa Yanga, ningempotezea tu. Tukio alilolifanya halikuwa la kiungwana. Ni vyema sasa akapambana na hali yake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’