Wachezaji Juma Abdul, Juma Mahadhi na Heritier makambo waliokuwa majeruhi Yanga wameanza mazoezi mepesi kuelekea kurejea dimbani
Mahadhi na Abdul walikosa mchezo wa mwisho wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports mapema wiki hii wakati Makambo aliumia kwa kuchanika nyama za paja kwenye mchezo huo uliopigwa nchini Rwanda.
Mahadhi amekuwa nje tangu alipoumia August 19 kwenye mchezo dhidi ya USM Alger huku Abdul akiumia mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mratibu wa klabu ya Yanga Hafidh Saleh amesema anaamini wachezaji hao watakuwa fiti kabla ya mchezo wa ligi dhidi ya Stand United, Septemba 16.
Kikosi cha Yanga kimeendelea kujifua uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam ambapo Jumatano ijayo, Septemba 05 watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United.
Mchezo huo utapigwa mkoani Kigoma kuwapa fursa wakazi wa mkoa huo ambao kwa takribani miaka 19 hawajashuhudia timu za ligi kuu zikicheza mkoani humo.

ADVERTISE HERE