Kombinesheni ya viungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Papy Tshishimbi, imekuwa tamu na kali ndani ya Ligi Kuu Bara kwa namna wanavyocheza, wakimrahisishia kazi straika Heritier Makambo ndani ya Yanga katika kutupia kambani.
Viungo hao wenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi za mabao kwa pamoja, huku Abdallah Shaibu ‘Ninja’ akicheza nyuma yao kwa lengo kuwapa uhuru na kumpigia pasi safi Makambo.
Hata hivyo, Fei Toto amefunguka na kudai licha ya kuelewana na Tshishimbi, lakini siku akitua Mohammed Issa ‘Mo Banka’ basi Makambo atakuwa anafunga sana na ikiwezekana kumfunika kabisa straika wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao matatu katika Ligi Kuu kwa sasa.
“Yanga itakuwa haishikiki katika safu ya kiungo kama Mo Banka naye akifika mapema tutakuwa tunaupiga mwingi na pasi za kumwaga kwa Makambo, ili aifanye kazi yake ya kufunga kwa ufanisi,” amesema Fei Toto.
Fei Toto aliongeza baada ya kucheza na Tshishimbi, amejikuta akijifunza vitu vingi ambavyo vitamsaidia katika uchezaji wake sasa na katika maisha yake ya soka kwa baadaye.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE