Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amerejea kwao DR Congo kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo yeye akiwa kocha msaidizi.
Baada ya kuiongoza Yanga kukamilisha mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho, licha ya kufungwa 1-0 na Rayon Sports, Zahera alisema kikosi chake kimeiva.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Zahera aliwasifu wachezaji wake kwa jinsi walivyopambana na kubainisha kuwa kama si mvua na upendeleo wa dhahiri uliofanywa na waamuzi wa mchezo huo, basi matokeo yangeweza kuwa tofauti.
Lakini jambo jema zaidi alilobaini baada ya mchezo huo ni kuimarika zaidi kwa kikosi chake.
Zahera amesema ana matumaini makubwa kuwa timu yake itafanya vizuri kwenye ligi na atahakikisha wanatwaa ubingwa msimu huu.
Mcongo huyo mwenye uraia wa Ufaransa amesema wachezaji Yanga wameiva na wamempa wigo mpana wa kuamua nani acheze katika kikosi cha kwanza.
"Ukiangalia mchezo dhidi ya Rayon, tuliwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na majeruhi huku wengine wakiwa hawajasajiliwa kwa ajili ya michuano hii."
"Lakini tulicheza vizuri. Tumedhihirisha kwamba timu yetu sasa imekamilika," alisema Zahera.

ADVERTISE HERE