Wachezaji wa Yanga wametamka kwamba kutolewa katika Kombe la Shirikisho Afrika kumewaimarisha na sasa akili yao ni kusaka taji la Ligi Kuu Bara ambalo linashikiliwa na Simba.
Pia, kocha Mwinyi Zahera amefunguka jinsi alivyokisuka kikosi chake na kwamba, suala la ubingwa mwishoni mwa msimu halina ubishi huku akionya kuwa Simba inabebwa na fedha tu kwa sasa ila haiwezi kuwa na maajabu kwa Yanga.
Hata hivyo, amesema kuwa Yanga inakabiliwa na tatizo moja tu kwa sasa na kama mabosi wake watalipatia ufumbuzi basi hakuna timu ya kushindana nayo kwenye Ligi Kuu Bara na itaingia kwenye klabu 10 bora Afrika.
Aliyeanza kutamka hayo kwenye mahojiano maalumu na gazeti la Mwanaspoti ni straika Ibrahim Ajib, ambaye alisema sasa wanarudi nyumbani kurudisha heshima kwa kuusaka ubingwa.
Ajib, ambaye ameacha gumzo nchini Rwanda kwa kuonyesha kiwango bora, alisema akili yao ni kuhakikisha wanalirudisha taji la ubingwa na kupambana mechi moja baada ya nyingine.
“Tunarudi nyumbani kurudisha akili yetu katika ubingwa, kwa sasa tumejifunza na tumeimarika kupitia mechi hizi.
“Binafsi sasa najiona niko sawa na siri kubwa ni mazoezi makali tuliyofanya lakini pia kutuliza akili yangu na kumtanguliza Mungu.”
Mbali na Ajib beki Andrew Vincent ‘Dante amesema kuwa wanatambua kuwania ubingwa watakuwa na vita na Simba na Azam, lakini wao watatumia ubora wao walionao sasa kurejesha heshima.
Dante alisema Simba ni timu nzuri lakini kwa sasa wanataka kushinda kila mchezo hadi kieleweke na kurudisha ubingwa nyumbani.
“Simba wana timu nzuri tunawaheshimu, lakini hata sisi sasa tuko sawa pengine kuliko msimu uliopita, tunarejea kutafuta ubingwa,” alisema Dante.
“Tutatumia ubora wetu kutafuta ubingwa hatutakuwa tunaiangalia Simba na mechi zao acha wao washinde na sisi tushinde alafu mwisho tutakutana.”
Kwa upande wa kocha Zahera amesema tangu amejiunga na Yanga amebaini mambo mengi makubwa na anaamini kama yatafanyiwa kazi basi itakuwa miongoni mwa timu bora Afrika.
Zahera amesema Yanga ina wachezaji wazuri na wenye uchu wa mafanikio, lakini ukata wa fedha ni kikwazo na unawakatisha morali na kushindwa kufikia mafanikio.
Amesema ameikuta Yanga ikiwa katika mazingira magumu, lakini imekuwa na wachezaji wengi wazuri wanaoelewa nini anakifundisha na kubainisha kuwa, wamekuwa wakimjengea sifa kubwa kutokana na kufanya anachowafundisha.
“Unajua Yanga ni timu kubwa nilikuwa naisikia hata kabla sijafika hapa kuifundisha, lakini ina changamoto moja tu na ndiyo inakwamisha ishindwe kufikia mafanikio, ni ukosefu wa pesa za kuendesha timu ya ushindani. Japo mabosi zangu wanajitahidi sana, lakini hawapaswi kuwa hapo walipo sasa,” alisema.
“Nimewakuta Yanga wakiwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ni timu ambayo imeruhusu mabao mengi ya kufungwa sio kuwa hawana wachezaji wazuri, hapana wapo lakini wanakosa maandalizi mazuri kama ilivyo kwa wawakilishi wengine,” alisema.
Zahera aliongeza kuwa endapo uongozi utahitaji kuwa na matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji, basi wanatakiwa kujenga ukaribu na kuwapa nafasi ya kuzungumza shida zao na kuzitatua kwa wakati ili kujenga mzuka muda wote.
Alisema kwa muda mchache aliokaa nao amebaini vipaji vingi na mapungufu madogo madogo waliyonayo, anaweka wazi kuwa ni mepesi kutatuliwa kama ataendelea kupewa muda wa kukaa nao kambini kwa muda wakifanya maandalizi.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE