Yanga imehitimisha michuano ya kombe la Shirikisho kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rayon Sports katika mchezo ambao matokeo yoyote yasingebadili chochote.
Yanga tayari ilikuwa imepoteza matumaini ya kutinga robo fainali. Hivyo mchezo wa leo ulikuwa wa kukamilisha ratiba tu.
Baada ya mchezo wa leo Yanga haitashiriki michuano ya CAF kwa msimu huu kwani ilishindwa kupata tiketi msimu uliopita.
Ukosefu wa fedha ndio sababu kubwa iliyopelekea Yanga ishindwe kufanya vizuri na wala sio swala la ubora wa kikosi chake.
Kocha Mwinyi Zahera ameweza kukifanya kikosi cha Yanga kuwa cha ushindani na hii ni baada ya wachezaji kutimiziwa mahitaji yao.
Kwa kuwa Yanga haishiriki mashindano ya CAF msimu huu, basi ni vyema timu ikajipanga kikamilifu hasa kiuchumi kuhakikisha inaporejea kwenye mashindano haya misimu ijayo isikumbwe na changamoto zilizojitokeza.
Aidha kocha Zahera amedhihirisha ni kocha mzuri na anaweza kuipa mafanikio Yanga siku za usoni.
Kama atapewa fedha za kusajili wachezaji anaowataka, anaweza kufanya muujiza.
Kwani amedhihirisha anao uwezo wa kutengeneza timu ya ushindani ambayo inaweza kuogopwa Afrika.

ADVERTISE HERE