Rayon Sports imefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga.
Bao pekee la Rayon lilifungwa na Bimenyimana kwenye dakika ya 19 kipindi cha kwanza.
Yanga ilikosa nafasi kadhaa kwenye kipindi cha kwanza huku ikionyesha kandanda safi kwenye kipindi cha pili licha ya mazingira mabaya ya uwanja wa Nyamirambo ambao ulifurika maji baada ya mvua kunyesha.
Rayon imeungana na USM Alger ambayo imeilaza Gor Mahia mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa dimba la Julai 05 huko Algeria.
USMA imemaliza kinara wa kundi D ikiwa na alama 11 ikifuatiwa na Rayon Sports yenye alama tisa.
Gor Mahia iliyokuwa kileleni kabla michezo ya leo imemaliza nafasi ya tatu ikijikusanyia alama nane wakati Yanga imemaliza mkiani ikiwa na alama nne.

ADVERTISE HERE