Leo saa kumi kamili jioni kwa saa za Tanzania, mabingwa wa kihistoria wa Tanzania, Yanga watashuka kwenye uwanja wa Nyamirambo nchini Rwanda kuumana na Rayon Sports katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho.
Yanga iko nchini Rwanda tangu jana Asubuhi ambapo jioni ilifanya mazoezi kwenye uwanja wa Nyamirambo utakaotumika katika mchezo wa leo.
Mshambuliaji Mcongo Haritier Makambo anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo huo.
Makambo amekuwa akizungumza zaidi na mashabiki nchini Rwanda kuelekea mchezo huo kutokana na uwezo ulioonyesha kwenye mchezo dhidi ya USM Alger.
Ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Yanga dhidi ya USMA umewafanya mashabiki wa Rayon kuingia hofu hasa ikizingatiwa timu yao inahitaji kushinda ili kusaka nafasi ya kutinga robo fainali.
Aidha, kikosi cha Rayon pia kinakabiliwa na changamoto baada ya shirikisho la soka Barani Afrika CAF kuwafungia wachezaji wake watatu muhimu Yanick Mukunzi, mlinda lango Kassim Nzayisenga na mshambuliaji Chris Mbonci.
Yanga nayo itawakosa wachezaji wake muhimu kama Juma Abdul na Papi Tshishimbi ambao hawakusafiri na timu kutokana na sababu mbalimbali.
Michezo kati ya Rayon dhidi ya Yanga na ule wa USM Alger dhidi ya Gor Mahia yote itapigwa kwa wakati mmoja ili kuepuka upangaji wa matokeo.
Gar Mahia inaongoza kundi D ikiwa na alama nane sawa na USMA lakini Gor iko kileleni kutokana kufunga mabao mengi kuliko USMA licha ya timu zote kuwa na uwiano sawa wa tofauti ya mabao (GD).
Rayon iko nafasi ya tatu ikiwa na alama sita. Kama itaibuka na ushindi dhidi ya Yanga halafu Gor Mahia itapoteza dhidi ya USMA nchini Algeria basi Rayon itafuzu.
Kwa kiasi kikubwa leo Yanga ndio itakayoamua hatma ya nani anafuzu kati ya Gor Mahia na Rayon. Matokeo ya sare au ushindi kwa Yanga yataivusha Gor Mahia hata kama itafungwa.
Gor Mahia ina nafasi finyu ya kuifunga USMA leo inayocheza kwenye dimba lake nchini Algeria.

ADVERTISE HERE