Michuano ya ligi ya mabingwa barani Africa hatua ya makundi inamalizika leo huku baadhi ya timu zikiwa tayari zimejihakikishia kutinga robo fainali.
Kundi A vilabu vya Al Ahly na ES Tunis tayari vimejihakikishia kutinga robo fainali ya michuano hiyo ambayo mshindi wake atajinyakulia kitita cha Bilioni nane baada ya kuongoza kundi hilo na vimefuzu kabla ya michezo yao ya mwisho leo.
TP Mazembe na ES Setif zimefuzu kutoka kundi B. Difaa El Jadida anayocheza winga wa zamani wa Yanga Simon Msuva imeshindwa kufuzu baada ya leo kulazimishwa sare bao 1-1 na TP Mazembe.
Kundi C, WAC Casablanka tayari imefuzu huku Horoya na Mamelodi Sundowns zikichuana kuwania nafasi ya pili. Horoya inahitaji alama moja tu iweze kufuzu huku Sundowns, mabingwa wa Afrika Kusini wakihitaji ushindi.
Kundi D, Etoile Du Sahel na 1st De Agosto zimefuzu robo fainali huku ZESCO inayonolewa na George Lwandamina, kocha wa zamani wa Yanga ikishindwa kupenya baada ya leo kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Etoile Du Sahel.
Michuano ya kombe la Shirikisho hatua ya makundi itafikia tamati kesho Yanga ikiwa nchini Rwanda kukamilisha ratiba kwa kuchuana na Rayon Sports.
Yanga yenye alama nne haina nafasi ya kutinga robo fainali lakini ushindi utaifanya iweze kumaliza nafasi ya tatu kundi D.

ADVERTISE HERE