Baada ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports keshokutwa, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera atakwenda DR Congo kutimiza majukumu ya kuinoa timu ya Taifa hilo imefahamika.
Licha ya kuinoa Yanga, Zahera bado ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo ambayo itakuwa na mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019 ambapo Septemba 09 itacheza na Liberia.
Hii ina maana kocha Msaidizi Noel Mwandila ndiye atakayekiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa raundi ya pili ya ligi kuu ya Tanzania Bara, Septemba 02 dhidi ya Mwadui FC mkoani Shinyanga.
Katika hatua nyingine, kibali cha kocha huyo inaelezwa kuwa kiko katika hatua za mwisho kukamilika na sasa kuna uhakika Zahera ataweza kukaa kwenye benchi atakaporejea kutoka DR Congo baada ya kukamilika kwa kalenda ya michezo ya Kimataifa

ADVERTISE HERE