Yanga yajihadhari kusajili 'magalasa' dakika za majeruhi

Yanga Damu By Yanga Damu
•
12 Aug 2017
Yanga yajihadhari kusajili 'magalasa' dakika za majeruhi
Mabingwa wa Tanzania, Yanaga sasa wameweka wazi kuwa, wapo makini kuelekea dakika za mwisho za usajili wa wachezaji wa kigeni kwa kuhakikisha hawasajili magarasa kama ilivyotokea huko nyuma kwa mitego waliyokuwa wakiwekewa.

Usajili kwa wachezaji raia wa Tanzania umemalizika tangu Agosti 6, mwaka huu, lakini Yanga ina nafasi ya kusajili mchezaji mmoja wa kigeni hadi Agosti 15 ambapo usajili huo utafungwa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amesema kipindi hiki wameamua kuwa makini zaidi ili kuepuka kusajili wachezaji wenye uwezo mdogo ambao huwaghalimu.

“Kuna wachezaji walikuja kwa ajili ya kufanya majaribio na tumeona hawana uwezo hao ni Mnigeria, Henry Okoh na Mcameroon, Ferdinand Bongyang ambaye tunamrudisha kwao muda wowote.

“Kwa sasa amebaki Yisa Mfowoshe ambaye ni Mnigeria huyu anaendelea kuangaliwa na tunasubiri majibu ya benchi la ufundi kama wameridhika naye ndiyo tujue mchakato wa kumsajili.

“Kumekuwa na tabia za mawakala kuleta wachezaji katika dakika za mwisho kwa ajili ya kufanya majaribio ambapo wamekuwa wakiangaliwa haraka haraka kisha wanasajiliwa.

“Huu ni mtego unaofanywa makusudi ili tuwasajili haraka bila kutathimini kwa kina uwezo wao, sasa tumeamua kuwa makini zaidi na suala hilo ili kusajili wachezaji wenye viwango na si vinginevyo,” alisema Mkwasa.

Wakati huohuo, kiungo mkabaji wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kuwasili nchini leo Jumamosi tayari kukitumikia kikosi hicho.

Tshishimbi raia wa DR Congo anawasili nchini baada ya Yanga kumalizana na klabu yake ya Mbabane Swallows ya Swaziland.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →