Mfumo wa viingilio kwenda kwa mwenyeji kuziumiza timu 'ndogo'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2018
Mfumo wa viingilio kwenda kwa mwenyeji kuziumiza timu 'ndogo'
Utaratibu wa kugawana mapato ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu wa 2018/19 umebadilishwa ambapo timu mwenyeji itachukua mapato yote ya mlangoni.

Tayari utaratibu huo umeanza kutia hofu kuwa utaziumiza baadhi ya timu hasa zenye mashabiki wachache.

Msemaji wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema utaratibu huo utazinufaisha baadhi ya timu ambazo zina wigo mpana wa mapato na mashabiki wengi.

Aidha kukosekana kwa mdhamini wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu inatajwa kuwa sababu nyingine ambayo itaziumiza timu kama utaratibu wa kugawana mapato hautatizamwa upya.

"Sisi (Mtibwa Sugar) hatuna tatizo kwa sababu timu yetu inaendeshwa na kampuni, lakini utaratibu huu ni pigo kwa timu zenye mashabiki wachache," alisema Kifaru.

"Mashabiki hawajitokezi kwa wingi huko mikoani isipokuwa zinapokwenda kucheza timu kama Yanga, Simba na pengine Azam FC, Mtibwa Sugar na Singida United."

"Timu hizi zenye mashabiki wachache hazitamudu gharama za uendeshaji," amesema.

Mabadiliko hayo ya mapato kuchukuliwa na timu mwenyeji yanaelezwa kuwa ni mapendekezo ya timu shiriki za ligi kuu ya Tanzania.

Hata hivyo uamuzi huo ulifikiwa wakati kukiwa na matarajio kuwa ligi hiyo ingekuwa na mdhamini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
2m ago
READ MORE β†’
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
2h ago
READ MORE β†’
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
3h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
9h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
21h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1d ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1d ago
READ MORE β†’