Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuondoka kesho Jumatatu kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports, Abdallah Shaibu 'Ninja', beki aliyebadilishiwa majukumu na kocha Zahera na kuwa kiungo mkabaji, huenda akaukosa mchezo huo.
Shaibu alipata majeraha ya bega kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar. Mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mchezaji huyo kutoka Zanzibar amekuwa akikumbwa mara kwa mara na tatizo hilo la bega.
Daktari wa Yanga Dr Edward Bavu amesema Shaibu atafanyiwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha tatizo hilo linalojitokeza mara kwa mara.
"Tunazo taarifa kuwa tatizo hili lilianza kumpata akiwa bado anacheza ligi kuu ya Zanzibar,mara nyingine tuliliona kwenye kombe la Mapinduzi," Dk Bavu aliiambia tovuti ya daboten.
"Ni wazi kwamba tunaatakiwa kumfanyia uchunguzi wa kina kujua shida ya ndani iliyopo kwenye bega lake, tuna wasiwasi huenda nyama au misuli midogo inayozunguka bega haiko kwenye kiwango sawasawa ndiyo maana limekuwa likiachia mara kwa mara."
Yanga inakwenda Rwanda kukamilisha mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kombe la Shirikisho.
Yanga tayari haina nafasi ya kutinga robo fainali lakini ushindi kwenye mchezo huo utakaopigwa Jumatano saa kumi jioni kwa saa za Tanzania, utaifanya imalize nafasi ya tatu.

ADVERTISE HERE