Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam Jumatatu kwenda nchini Rwanda tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports.
Mchezo huo utapigwa Jumatano ijayo, August 29 huko Rwanda.
Baada ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo uliopita dhidi ya USM Alger, Yanga yenye alama nne inaweza kumaliza katika nafasi ya tatu kama itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
Rayon Sports ina alama sita na kama itashinda halafu Gor Mahia ikachapwa na USM Alger, Wanyarwanda hao wanaweza kupenya hatua ya robo fainali.
Hata hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani wa aina yake kutokana na ubora wa kikosi cha Yanga wakati huu lakini pia ushindi utaipeleka Yanga nafasi ya tatu na kuongeza kiasi cha fedha ambazo italipwa na CAF.
Mchezo huo utapigwa saa 10 jioni.

ADVERTISE HERE