Makambo awavulia kofia Fei Toto, Kakolanya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2018
Makambo awavulia kofia Fei Toto, Kakolanya
Mshambuliaji anayetajwa kuwa bora zaidi kwa wakati huu nchini Heritier Makambo amewasifu kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' na mlinda lango Beno Kakolanya kwa kiwango waliochoonyesha kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mtibwa Sugar.

Makambo ambaye alifunga moja ya mabao ya Yanga na kuifanikisha timu hiyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, amesema Kakolanya na Fei Toto walichangia kwa kiasi kikubwa Yanga kuibuka na ushindi.

"Hawa wawili waliifanya Yanga inawiri jana. Walikuwa bora sana kwenye nafasi zao. Mnastahili pongezi na muendeleze moto huo mlianza nao," amesema Makambo.

Licha ya umri wake wa miaka 19, Feisal tayari ameonyesha kuwa mmoja wa viungo bora kabisa. Kwa kushirikiana na Tshishimbi, Ajib na Kaseke, viungo hao wlaifanikiwa kutawala mchezo hasa kwenye kipindi cha kwanza



Mlinda lango Beno Kakolanya kwa mara nyingine jana ameonyesha kuwa anastahili kuwa namba moja sasa.

Aidha hakuna shaka Mkufunzi wa timu ya Taifa Emanuel Amunike ambaye jana alikuwepo uwanjani, amejipongeza kwa kumuita Kakolanya kwenye kikosi chake kitakachoivaa Uganda Cranes Septemba 08.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
47m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’