Kuna taarifa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera huenda asiwepo kwenye benchi leo wakati timu yake itakapocheza na Mtibwa Sugar uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara kutokana na kutokamilika kwa mchakato wa kupata kibali cha kufanya kazi nchini.
Hivi karibuni uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Hussein Nyika ulitoa taarifa kuwa maombi ya kibali cha kocha huyo mchakato wake ulikuwa mbioni kukamilika.
Nyika alisema moja ya changamoto zilizopelekea kuchelewa kupatikana kwa kibali cha Zahera ni kutokana na ofisi za Uhamiaji kuhamia Dodoma.
"Tulimtuma kijana wetu kwenda kufuatilia mkoani Dodoma. Tayari amerejea na mchakato uko katika hatua za mwisho kabisa," alisema Nyika
Zahera amekuwa nchini kwa karibu miezi minne, WanaYanga wamekuwa wakijiuliza kulikoni mpaka leo bado hajapata kibali?

ADVERTISE HERE