Kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya kiungo fundi Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Kuna tetesi kuwa viongozi wa Simba wamempa ofa na Mil 100 asaini katika klabu hiyo. Taarifa hizi sio za kweli.
Ni kweli Niyonzima bado hajasaini mkataba mpya na Yanga lakini sio kweli kuwa Simba wamemsainisha tayari.
Niyonzima aliahidi kuwa punde akirejea atasaini mkataba mwingine kuendelea kuitumikia Yanga .
Makubaliano yaliyofikiwa ni Niyonzima kusaini mkataba wa miaka miwili,hata hivyo viongozi wa Simba wanadaiwa kumtumia mkewe ambaye yuko nchini amshawishi Niyonzima asaini Simba.
Ni kama Simba inataka kulipa kisasi baada ya kumpoteza Ibrahim Ajib.
Niyonzima ana mapenzi makubwa na klabu ya Yanga na atasaini mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga.
Viongozi wa Simba wamekuwa wakiwapa matumaini mashabiki wao ili waamini kuwa timu yao inafanya kila linalowezekana kumpata Niyonzima.

ADVERTISE HERE