Mmoja wa wachezaji waliomwagiwa sifa kedekede baada ya mchezo wa juzi dhidi ya USM Alger ni mlinda lango Benno Kakolanya.
Kakolanya alionyesha kwa nini anastahili kuaminiwa kulinda lango la Yanga.
Msimu uliopita hakuonekana sana dimbani sababu kubwa ikiwa ni majeraha ya goti yaliyokuwa yakimsumbua. Lakini pia kuaminiwa kwa Rostand ilikuwa kikwazo kwake.
Kindoki au Kakolanya?
Baada ya kuachana na Youthe Rostand, Yanga ilimleta mlinda lango kutoka DR Congo Klaus Kindoki. Uamuzi huo unaonekana kuinufaisha Yanga.
Katika michezo kadhaa ya kirafiki aliyocheza, Kindoki ameonyesha uwezo wa hali ya juu.
Hakika, benchi la Ufundi la Yanga litakuwa na wakati mgumu kuamua nani awe namba moja na nani awe namba mbili.
Misimu mitatu nyuma, Yanga iliwahi kuwa na walinda lango watatu mahiri kwa wakati huo, Juma Kaseja, Ali Mustafa na Deo Munishi.
Ni wakati huo ambao Yanga ilikuwa na utulivu mkubwa langoni.
Hans van Pluijm akiwa ndiye mkufunzi wa Yanga kipindi hicho, alikuwa akibadilisha mlinda lango kila baada ya michezo kadhaa ili kuwafanya 'wasibweteke'.
Huenda hali hiyo ikajirudia msimu huu.

ADVERTISE HERE