Sababu ya mchezo wa Ruvu Shooting kuhamishiwa uwanja wa Chamazi

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
11 Aug 2017
Sababu ya mchezo wa Ruvu Shooting kuhamishiwa uwanja wa Chamazi
Akizungumza na waandishi wa Habari leo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting umehamishiwa uwanja wa Chamazi kutokana na Uwanja wa Taifa kesho kutumika kwa shughuli za kiserikali.

"Tumepata taarifa kutoka serikalini asubuhi kuwa Uwanja wa Taifa kesho unatumika kwa shughuli za kitaifa hivyo hatutaweza kucheza mechi yetu hapo na kama unavyojua hatuwezi kubishana na Serikali.

"Tunaishukuru Azam kwa kutukubalia mechi yetu tuihamishie kwenye uwanja wao, hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi Chamazi kushuhudia mchezo huo kama walivyofanya katika mchezo uliopita," alisema Mkwasa.

Alisema katika mchezo huo viingilio vitakuwa Sh7,000 kwa VIP na Sh5,000 mzunguko.

Mkwasa alisema baada ya mchezo huo wa kesho, Yanga itaondoka Jumapili asubuhi kwenda Zanzibar na usiku itacheza mechi nyingine ya kirafiki na Mlandege itakayofanyika kwenye Uwanja wa Aman .

Alisema Jumatatu timu hiyo itaelekea Pemba kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba itakayofanyika Agosti 23.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’