Mgeni rasmi wa mchezo wa kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya USM Alger, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo, amewapongeza wachezaji wa Yanga kwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.
Yanga imeilaza USM Alger mabao 2-1, huo ukiwa ni ushindi wake wa kwanza kwenye michuano hiyo.
Jenerali Mabeyo amesema amefarijika kwa ushindi huo na amefurahi zaidi kwa kuwa ugeni wake umekuwa na baraka.
"Nimefarijika kwa mchezo mzuri mlioonyesha. Kikubwa nashukuru ugeni wangu umeleta matunda," amesema Jenerali Mabeyo.
Naye Meneja wa Yanga Nadir Haroub amemshukuru mgeni rasmi Jenerali Mabeyo kwa kukubali kuhudhuria mchezo huo.
Nadir amesema wachezaji wamepata hamasa kubwa kutokana na uwepo wao dimbani.
Pia amemshukuru mgeni rasmi pamoja na uongozi wa Yanga chini ya Mwenyekiti Yusufu Manji kwa kuwapa kifuta jacho baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi leo.

ADVERTISE HERE