Tujitokeze kwa wingi uwanja wa Chamazi Jumamosi

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
11 Aug 2017
Tujitokeze kwa wingi uwanja wa Chamazi Jumamosi
Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga kesho Jumamosi, August 12 wanashuka dimbani kwenye uwanja wa Chamazi kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ruvu Shooting.

Huo ni mchezo rasmi wa kirafiki wa pili baada ya ule wa wiki iliyopita dhidi ya Singida United na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amewaasa mashabiki na wanachama wa Yanga kufika kwa wingi kwenye dimba la Taifa kuona maendeleo ya timu yao kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea visiwani Zanzibar siku ya Jumapili, August 13 ambapo saa moja jioni siku hiyo hiyo itacheza mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Mlandege.

Baada ya mchezo huo Yanga itaingia mafichoni kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba August 23.

Katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting huenda kiungo mpya Papi Tshishimbi pamoja na mlinzi wa kati Yisha Anifowoshe aliye kwenye majaribio, wataichezea Yanga kwa mara ya kwanza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’