FT : Yanga 2-1 USM Alger

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2018
FT : Yanga 2-1 USM Alger
Yanga imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuilaza USM Alger mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Taifa.

Ikicheza kwa umakini na tahadhari kubwa, Yanga ilioonyesha kubadiliki kabisa, ilikuwa hatari zaidi kwenye mashambulizi ya kushitukiza.



Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Deus Kaseke kwenye dakika ya 43 baada ya kuwahi mpira uliopigwa na mlinzi wa USMA aliyetaka kumrudishia mlinda lango wake.

Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, mfumo wa kujilinda na kushambulia pamoja uliotumiwa na kocha Mwinyi Zahera uliifanya Yanga iwe na ukuta mgumu uliowapa wakati mgumu USMA kuupenya.

Bao la pili la Yanga lilifungwa na Heritier Makambo aliyewahi pasi 'mpenyezo' iliyopigwa na Deus Kaseke.

USMA ilifunga bao lake kupitia kwa Abderahmane kwenye dakika ya 53 akipiga shuti nje ya 18 baada ya walinzi wa Yanga kuchelewa kumkaba.

Ushindi huo umewanyamazisha wakosoaji wengi waliokuwa na matokeo mfukoni kabla ya mchezo kupigwa.



Ndio, Manji karudi

Matokeo hayo pia yamenogesha kurejea kwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusufu Manji ambaye alikuwepo kwenye dimba la Taifa kuushuhudia mchezo huo.

Mapema alipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji akawahamasisha na hakuna shaka tukio hilo alilolifanya liliongeza morali ya wachezaji.

Tatizo letu sio wachezaji

Matokeo ya mchezo wa leo yamedhihirisha Yanga ingefanya vizuri kwenye michuano hii kama kungekuwa na utulivu wa kiuchumi.

Leo wachezaji wameonyesha kujiamini na hakika kwa wale waliokuwa wanadhani Yanga ni mbovu leo wameiona na huko waliko watakuwa wamepatwa na matumbo ya kuhara...!

Pamoja na maandalizi mazuri, utulivu wa wachezaji ni jambo muhimu kwa timu kuweza kufanya vizuri.

Zahera yuko vizuri

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekaa kambini na wachezaji kwa siku 10 tu mkoani Morogoro lakini anastahili pongezi kwa kazi kubwa aliyofanya.

Leo tumeishuhudia Yanga yenye nidhamu ya hali ya juu kwenye ulinzi. Uamuzi wake wa kumtumia Abdallah Shaibu 'Ninja' kama kiungo mkabaji umeongeza ugumu kwenye safu ya ulinzi.

Mchezo wa leo dhidi ya USMA ulikuwa kipimo sahihi kwa kocha Zahera. Wapo walioibeza Yanga kuwa imecheza michezo rahisi ya kirafiki.

Lakini kwa matokeo ya leo, inadhirisha kwa muda mfupi amefanikiwa kutengeneza kikosi imara.

Gor Mahia nao wamepigwa 2-1 na Rayon Sports

Wakati Yanga ikishinda Dar, Gor Mahia imechapwa mabao 2-1 na Rayon Sports kwenye mchezo mwingine uliopigwa huko Kenya.

Yanga itasafiri wiki ijayo kwenda Rwanda kuikabili Rayon Sports kwenye mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi.

Rayon Sports imefikisha alama sita baada ya kushinda leo, ina nafasi ya kutinga robo fainali kama itashinda mchezo dhidi ya Yanga.

Hata hivyo Yanga yenye alama nne itahitaji kushinda mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya tatu na kuongeza 'mkwanja'
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’