Manji ateta na wachezaji, viongozi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2018
Manji ateta na wachezaji, viongozi Yanga
Jana Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yususfu Manji alikutana na wachezaji na viongozi wa Kamati ya Mashindano ya Yanga kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mpambano wa leo kukamilisha ratiba dhidi ya USM Alger.

Mpema jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hussein Nyika alisema kamati yake ilifanya kikao na mwenyekiti wao, ambaye alikuwa nje ya soka kwa muda mrefu na amewahakikishia atakuwepo uwanjani hapo leo.

Jana usiku, Manji alipata chakula pamoja na wachezaji na viongozi, pia alizungumza na wachezaji.

β€œManji ameahidi atakuwepo uwanjani leo hivyo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kuiona timu na kumwona kiongozi wao na tuna imani kubwa kufika kwake ni mwanzo mzuri kwetu na baada ya hapo tutafanya mengine zaidi ya kimaendeleo,” alisema Nyika.

Naye Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kikosi na wachezaji wote ambao wana leseni ya kushiriki mashindano hayo wapo fiti na jukumu litabaki kwa Zahera kuamua nani wa kumtumia katika mechi hii.

Ten alisema viingilio vitakuwa Sh3,000, kwa mzunguko VIP B na C itakuwa Sh7,000 wakati VIP A itakuwa Sh10,000 na tuna imani viingilio rahisi kwa kila mpenzi wa soka kuja kushuhudia burudani.

β€œMgeni rasmi kama kawaida atakuwa Jenerali Venance Mabeyo, pia tulimwalika Rais wetu John Pombe Magufuli, ambaye amekuwa akitupa ushirikiano wa kutosha, lakini hataweza kuhudhulia kutokana kuwa na majukumu mengine ya kitaifa,” alisema Ten.

Yanga imepata mzuka huo ikiwa pia inajiandaa na michuano ya Ligi Kuu inayotarajiwa kuanza Agosti 22 na itaanza kukipiga na mabingwa wa kombe la FA, Mtibwa Sugar ya Morogoro, August 23 kwenye uwanja wa Uhuru.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’