Makambo kuongoza 'jeshi' la Yanga leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Aug 2018
Makambo kuongoza 'jeshi' la Yanga leo
Leo Jumapili, August 19 2018 saa moja jioni Yanga itashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili USM Alger katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Yanga itatumia mchezo huo kupima uimara wa kikosi chake kabla ya kuanza kwa ligi kuu ya Tanzania Bara Jumatano ijayo.

Yanga itakayoivaa USM Alger leo itakuwa tofauti kabisa na ile iliyofungwa mabao 4-0 nchini Algeria kwenye mchezo wa kwanza.

Mshambuliaji mpya Heritier Makambo, aliyesajiliwa na Yanga kutoka FC Lupopo na DR Congo anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo huo.

Hii ni baada ya jina lake kuidhinishwa na CAF kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho sawa na Deus Kaseke na Matheo Anthony ambao wao waliweza kucheza mchezo uliopita dhidi ya Gor Mahia.

Yanga pia itakuwa na mabadiliko langoni ambao baada ya kuachana na Youthe Rostand, Benno Kakolanya anatarajiwa kuchukua nafasi yake.

Kurejea kwa nahodha Kelvin Yondani pia kunatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya Yanga.

Baada ya kambi ya siku 10 mkoani Morogoro, kikosi cha Yanga kimeimarika. Mchezo wa leo utakuwa kipimo sahihi kuelekea msimu mpya.

Manji kuongeza mzuka

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bilionea Yusufu Manji atakuwepo uwanjani kuushuhudia mchezo huo.

Mapema jana Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga Hussein Nyika alisema Manji atakuwa sehemu ya viongozi watakaokuwepo uwanja wa Taifa.

Mgeni rasmi wa mchezo huo ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo.

Yanga iliwasili kutoka Morogoro jana na kufikia hoteli ya Protea ambapo jioni wachezaji pamoja na viongozi walipata chakula pamoja.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’